Search This Blog

Wednesday, February 10, 2021

Marekani yarejea Baraza la Haki za Binadamu


Marekani imetangaza mpango wa kurejea katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ikiwa ni miaka mitatu  tangu Rais wa zamani, Donald Trump alipoitoa nchi hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa  Marekani, Antony Blinken amesema kuiondoa Marekani Juni 2018, hakukusaidia kuleta mabadiliko yoyote ya maana ila kulisababisha ombwe la Uongozi  ambalo Mataifa yenye ajenda za kimabavu yamelitumia kwa faida yao.

Uamuzi huo unaweza kukosolewa na Wabunge na raia wanaoiunga mkono Israel, ambao wamelikosoa Baraza hilo kwamba halichukulii kwa uzito ukiukaji wa Tawala na Serikali za Kimabavu, na linazikubali nchi husika kuwa wanachama.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...