Wakazi wa kaskazini mwa Uganda leo hii wanasubiri mahakama ya uharifu wa kimtaifa ICC kutowa hukumu ya kesi anayotuhumiwa aliyekuwa afisa wa kundi la wanamugambo wa LRA, bwana Domini Ogwen.
Dominic anakabiliwa na mashitaka 70 ya uhalifu wa kivita ukiwemo ubakaji wa wanawake na mauaji.
Waathiriwa wa vita vya wa waasi wa LRA wanatarajia mhakama ya ICC itawatendea haki.
Dominic Ogwen alikuwa kamanda wa kundi la waasi wa LRA linaloongozwa na Josephy Kony kuanzia mwaka 2014 mwishoni.
Dominic Ogwen alitoroka kufungwa na mkuu wake Josephy Kony baada ya kutofautiana na kukimbilia kwa waasi wa Jamuhuri ya Afrika kati , kiongozi wa Selika aliwasiliana na vikosi vya Marekani na kumuchukua Ogwen hadi kwa kikosi cha jeshi la Uganda kilichokuwa kikiwasaka waasi wa Kony walikuwa Jamuhuri ya Afrika ya kati
Kabla ya kukamtwa mahakama ya uhalifu wa kimtaifa ya ICC ilitowa waranti ya kukamtwa kwa viongozi wa kundi la waasi wa LRA mnamo June mwaka 2005 akiwemo Kiongozi wa kundi hilo Josephy Kony ,Dominic Ogwen na viongozi wengine wanne.
Ogwen baadaye alifikishwa mahakama ya ICC mwaka 2015 na kufunguliwa mashitaka 70, na sasa mahakama hiyo inatarajiwa kutowa hukumu leo.
Mmoja wa wahanga aliyetekwanyarwa na waasi wa Kony kwa muda mrefu anaomba mahakama kuwatendea haki.
Dominic Ogwen alizaliwa mwaka 1975 katika kijiji cha Choorum wilaya ya Amuru kaskazini mwa Uganda.alitekwenyara na kundi la waasi wa Josephy Kony akiwa mvulana mdogo wakati akielekea shule ya msingi Abili Koro, kulingana na maelezo yake alidai alitekwanyara mwaka 1988 akiwa na umri wa miaka 14.
Lakini ripoti sahihi zinasemekana alitekwanyara akiwa na umri wa miaka 9 au 10.
Kwani alibebwa katika safari yao hadi kwenye kambi ya LRA, alikuwa hawezi kutembea.
Mama yake Ogwen alipofahamishwa habari za kutekanywara kwa mtoto wake aliamuwa kuwafata wafuasi hao, na badaye watu walimkuta mama huyo amefariki pamoja na mumewe.
Baada ya muda akiwa na umri wa miaka 18, Ogwen alipewa cheo cha Brigadier wa kundi la waasi wa LRA na kuongoza kikosi cha Sinia.
Ogwen alishirika katika matukio mbalimbali ya uhalifu wa kivita mwezi wa Mei mwaka 2004 walishambulia kambi ya ndani ya Lukodi wilayani Gulu kaskazini mwa Uagnda.
Pia alishambulia kambi nyingine za ndani ikiwemo ya Pajule, Odeke na Abok na kushiriki mauaji mbalimbali ya waanchi wasiokuwa na hatia , ubakaji na unyanyasaji wa kigono.

No comments:
Post a Comment