Maelfu ya Watunisia walikiuka amri ya polisi na walijitokeza katika barabara za mji mkuu wa Tunis ili kuadhimisha miaka minane tangu mauaji ya kiongozi wa kisiasa wa mrengo wa kushoto Chokri Belaid.
Mnamo Februari 6, mwaka 2013 Chokri Belaid aliuwawa nje ya nyumba yake na miezi sita baadaye kiongozi mwingine wa mrengo wa kushoto, Mohammed Brahmi pia aliwawa na kusababisha Tunisia kuingia katika machafuko wakati huo.
Hakuna mtu yeyote alikamatwa au kuhukumiwa kwa kesi za mauwaji ya viongozi hao. Waandamanaji katika maadhimisho hayo walikua wakiimba wakisema kuwa mitaa inamilikiwa na watu na kukiuka agizo la polisi na kuandamana kuelekea katika eneo badilishwa jina Belaid kama kumbukumbu ya kumuenzi.
Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi, Hamma Hammami, amekilaumu Chama cha Kiislamu Ennahda, ambacho kiliongoza serikali ya Tunisia wakati wa mauaji ya Belaid dhidi ya Uisilamu kwamba chama hicho kimeendelea kujikwaa na kupunguza kasi ya mahakama katika mchakato katika kesi hiyo.

No comments:
Post a Comment