Kocha mpya wa klabu ya Simba, mfaransa Didier Gomez Da Rosa amejinasibu kupata ushindi ugenini dhidi ya klabu ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa kiporo wa ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa saa 10:00 jioni ya leo tarehe 4 Februari 2021 kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Kuelekea kwenye mchezo huo ambao ni wa kwanza kwa kocha huyo kwenye VPL, Didier amesema “ni mchezo muhimu kushinda na tutatshinda. Tuna michezo mitatu mfululizo ijayo na ni muhimu kuanza kushinda na huu. Tupo nyuma ya Yanga kwa alama 9 hivyo tunakilasababu ya kuzipunguza”.
“Tutapambana kucheza na kushinda kabla ya kucheza na Azam kwenye mchezo ujao”. Didier akamaliza kwa kusema hivyo.
Simba huenda isiwe kikosini na nahodha wake, mshambuliaji John Bocco licha ya kuanza mazoezi mepesi tokea alipokuwa na timu ya taifa 'Taifa Stars' kwenye michuano ya CHAN inayoendelea nchini Cameroon ambapo Bocco alishindwa kucheza mchezo hata mmoja kwasababu ya kuwa na majeraha.
Kwa upande wa wenyeji wa mchezo huo, Kocha wa klabu ya Dodoma Jiji, Mbwana Mkata amesem a anatazamiwa kuwakosa wachezaji wake wawili kutokana na majeraha, mshambuliaji Seif Karihe ambaye aliwania tuzo ya mchezaji bora wa mwezi disemba baada ya Omary Rajabu.
Baada ya mchezo huo kumalizika, kikosi cha Simba kinatazamiwa kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam alfajiri ya siku ya kesho Ijumaa tarehe 4 Februari 2021 kwa ndege kwa ajili ya maandalizi ya mchezo unaofuata dhidi ya Azam utakaochezwa siku ya Jumapili tarehe 7 Februari 2021.
Simba ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza michezo 15, 3 nyuma ya Yanga na kujizolea alama 35, alama 9 nyuma ya vinara Yanga ilhali Dodoma Jiji ipo nafasi ya 10, alama 22 baada ya kucheza michezo yake 22.
Mchezo mwingine wa VPL utakaochezwa saa 10:00 jioni ya leo ni KMC ambao watawakaribisha Namungo kwenye dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment