Search This Blog

Saturday, February 13, 2021

Kamati ya Siasa CCM Dodoma Mjini yaja kivingine ukaguzi wa miondombinu ya barabara


Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Dodoma imekuja na njia mpya ya kuhakikisha huduma ya miondombinu ya usafiri inaboreshwa kwa kufanya ziara na Wakala wa barabara za Mjini na vijijini TARURA katika maeneo yote korofi yanayolalamikiwa na wananchi kutopitika hasa katika kipindi hiki cha mvua.

Ikiwa ni mwendelezo wa ziara ya kamati ya siasa kukagua miradi na huduma za kijamii  imetembelea maeneo mbalimbali ya jiji la Dodoma ambayo miondombinu yake si rafiki kwa watumiaji kutokana na kuharibika vibaya.

Kamati imepita na kukagua barabara ya Ihumwa inayounganisha barabara kuu ya Morogoro na stesheni ya treni ya kisasa  inayojengwa katika eneo la Ihumwa barabara ambayo imeharibika kutokana na kutumika na magari makubwa yanayofikisha vifaa vya ujenzi katika stesheni ya Treni.

Barabara nyingine ni barabara za kata ya Nzuguni ambazo baadhi yake zinalalamikiwa na wananchi kutopitika kabisa kutokana na ubovu, barabara za kata ya kilimani katika eneo la Chinyoya ambazo pia hazipitiki, barabara za kata ya Kikuyu na baadhi ya barabara katika eneo la Mtaa wa Area C.

Ambapo Meneja wa TARURA Wilaya ya Dodoma Mhandisi Godlack Mbanga amesema TARURA imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha barabara zote katika Jiji la Dodoma zinapitika huku akibainisha kuwa changamoto ni baadhi ya barabara kutokusajiliwa hivyo kukosa bajeti lakini wamekuwa wakishirikiana na Jiji la Dodoma katika kuziboresha.

"Barabara nyingi zinaendelea kukarabatiwa na nyingine tayari wakandarasi wamesha saini mikataba tayari kwa ujenzi, changamoto ni baadhi ya barabara hazijasajiliwa lakini tunashirikiana na jiji kwa wao kutoa vifaa na sisi kuchangia mafuta ili barabara zote zikarabatiwe" amesema Mbanga.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...