Search This Blog

Tuesday, February 9, 2021

Jengo la makao makuu ya chama kinachoongozwa na Suu Kyi lavamiwa na jeshi Myanmar


Vikosi vya usalama vimevunja milango kwa nguvu majira ya jioni siku ya Jumanne. Hakuna wanachama wa chama waliokuwepo katika jengo hilo wakati huo.

Shambulio hilo linakuja wakati maelfu wakiendelea kupinga maandamano ya kijeshi ambayo yaliondoa NLD kutoka serikalini.

Wengi wanadai kuachiliwa kwa Bi Suu Kyi na washirika wakuu wa NLD.

Kwa sasa hawajulikani walipo na Bi Suu Kyi hajaonekana tangu mapinduzi ya mapema wiki iliyopita.

"Dikteta wa kijeshi alivamia na kuharibu makao makuu ya NLD karibu saa 9:30 alasiri," NLD ilitangaza kwenye ukurasa wake wa Facebook, ingawa haikutoa maelezo zaidi.

Uvamizi huo ulifanyika wakati wa amri ya kutotoka nje ya nchi nzima usiku, ambayo huchukua saa mbili usiku mpaka saa kumi alfajiri 04:00 kwa saa za nchi hiyo

Mikusanyiko ya zaidi ya watu watano pia imepigwa marufuku. Lakini waandamanaji wamepuuza hili kwa maelfu kuingia barabarani Jumanne kwa siku ya nne mfululizo na polisi kujibu kwa matumizi makubwa ya nguvu, na kusababisha majeruhi kadhaa yaliyoripotiwa.

Siku ya Jumatano asubuhi, kundi kubwa la watumishi wa Umma lilikusanyika katika mji wa Nay Pyo Taw. liliripoti gazeti la Myanmar Now



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...