Search This Blog

Monday, February 15, 2021

Jaji ataka aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma kufungwa gerezani


Jaji mmoja nchini Afrika Kusini amesema anataka aliyekuwa rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kuhukumiwa kifungo gerezani kwa kushindwa kufika mahakamani kujibu madai ya ufisadi.

Bwana Zuma, 79, alidharau ombi la kufika mbele ya tume ya uchunguzi ambayo mwenyekiti wake ni hakimu Ray Zondo.

Jaji amesema ukaidi wa Bwana Zuma kunaweza kusababisha kutotekelezwa kwa sheria na kwamba ataomba mahakama ya juu ya Afrika Kusini kumhukumu aliyekuwa rais kwa kosa la kukiuka masharti ya mahakama.

Bwana Zuma amesema anaamini kwamba jaji Zondo alikuwa na upendeleo katika uamuzi alioutoa dhidi yake.

Awali, alikuwa ametaka jaji huyo kujiuzulu kama mwenyekiti wa jopo la uchunguzi wa kesi dhidi yake.

Jaji Zondo alitupilia mbali ombi hilo na kusema anafanya kazi yake bila upendeleo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...