Search This Blog

Monday, February 8, 2021

Iran 'inaficha kifaa cha ujasusi kwenye kuta za nyumba na programu za mtandaoni


Iran inaendesha harakati za ujasusi katika mtandao, ikiwalenga zaidi ya wapinzani wake 1,000 , kulingana na kampuni maarufu zaidi ya usalama wa mtandao.

Juhudi za ujasusi huo zilielekezwa dhidi ya watu binafsi nchini Iran na katika nchi nyingine 12, ikiwa ni pamoja na Uingereza na Marekani , imesema kampuni ya Check Point.

Imesema kuwa makundi mawili yaliyohusika na ujasusi huo yalitumia mbinu mpya ya kuweka mtambo wa ujasusi kulenga kpmpyuta na simu za mkononi.

Halafu mitambo hii inatumiwa kuiba mawasiliano ya simu yaliyorekodiwa na picha pamoja na video zilizomo ndani ya kompyuta na simu.

Moja ya makundi, yanayofahamika kama Pusi wa nyumbani au APT-50, yanashutumiwa kwa kuwalaghai watu wapaukue programu za njama kwenye simu zao za mkononi kwa njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na:

Kuweka michezo kuweka upya video halisi za mtandaoni zinazopatikana katika programu ya Google Play

Kutoa programu ya mtandao bandia ambayo inachapisha taarifa kutoka mashirika ya habari nchini humo

Kusambaza karatasi za mapambo ya ukutani kama zawadi ambazo huwa zimewekwa vifaa vya udukuzi zenye picha za kupinga Islamic State

Kujifanya kama programu ya Android na kupakua programu nyingine zaidi za kompyuta au simu

Kampuni ya watafiti wa Kimarekani na Kiisraeli iliwabaini waathiriwa 1,200 ambao wanalengwa na harakati za ujasusi huo, wanaoishi katika nchi saba.

Kulikuwa na mafanikio zaidi ya 600 ya ujasusi huo, ilisema.

kikundi cha pili, kinachofahamika kama Infy au Prince Of Persia, kinasemekana kufanya ujasusi katika nyumba za makazi ya watu na katika kompyuta za wapinzani katika nchi 12, kwa kutoa data za siri baada ya kuwalaghai watu wafungue barua pepe zenye njama zao ambazo huwa zina ujumbe uliambatanishwa kwenye barua pepe.

Serikali ya Iran bado haijatoa kauli yoyote kuhusiana na ripoti za tuhuma za ujasusi huu dhidi yake.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...