Idadi ya vifo iliongezeka hadi 7 baada ya mtu mwingine mmoja kufariki kutokana na makabiliano ya vikosi vya usalama katika maandamano dhidi ya mapinduzi ya kijeshi yaliyoendelea nchini Myanmar.
Kulingana na taarifa za vyombo vya habari vya nchi, polisi waliingilia kati maandamano katika mji wa Monwya na kutumia risasi halisi na vilipuzi.
Wakati waandamanaji wengi walijeruhiwa kutokana na makabiliano ya polisi, mhudumu mmoja wa afya alifariki baada ya kulengwa risasi mwilini mwake.
Katika video zilizochapishwa na waandamanaji kwenye mitandao ya kijamii, ilionekana kuwa vikosi vya usalama vilipiga magoti na kuelekeza bunduki zao kwa kundi la waandamanaji.
Katika miji ya Yangon na Mandalay, kulikuwa na ushiriki mdogo kwenye maandamano hayo ya kupinga mapinduzi kutokana na vizuizi vya polisi vilivyowekwa kwenye maeneo ya wazi.
Katika maandamano hayo dhidi ya mapinduzi ambayo yamekuwa yakiendelea tangu Februari 6, mtu 1 alifariki mjini Yangon na wengine 5 mjini Mandalay kutokana na makabiliano ya vikosi vya usalama.

No comments:
Post a Comment