Search This Blog

Tuesday, February 16, 2021

Hamisa Mobetto amtaka Kajala amuombe radhi

 


Mwanamitindo na mwimbaji Hamisa Mobetto, kupitia wanasheria wake wa kampuni ya Mass Attorneys, amemtaka Kajala Masanja  amuombe radhi staa huyo kwa kumzushia uongo Jumapili ya Februari 14, 2021.

Kajala ametakiwa kufanya hivyo ndani ya saa 12 baada ya kupokea barua hiyo na kama asipotii, watamshtaki mahamakani.

Pia barua hiyo imesema, iwapo #Kajala atafuta post yake, kukanusha uzushi aliouandika na kumuomba radhi Hamisa, yatafuata mazungumzo ya kiasi anachotakiwa kumlipa mteja wao kutokana na hasara aliyomsababishia.

Kwenye post yake ya Instagram, Kajala alimshutumu #Hamisa kuwa baada ya kumchukua bintiye Paula kwenda kula lunch, alimkutanisha na Ray Vanny ambaye alimlewesha na kumrubuni kushoot video zisizo na maadili.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...