Kwa mujibu wa orodha ya hivi karibuni ya watu waliopata mafanikio kwa kuwa watu bora , kampuni ya Freddie Figgers cina thamani ya dola milioni 62, kitu ambacho alifanikiwa kwa kuwa mtu mwema na mwenye kipaji.
Alipokuwa mtoto mchanga, Figgers alitupwa karibu na pipa la takataka katika eneo la vijijini la Florida nchini Marekani
"Watoto walikuwa wakimcheka, walikuwa wakimuita 'mtoto takataka', walimwambia 'hakuna mtu anayeku[penda wewe…wewe ni mchafu '.
''Nakumbuka nyakati fulani nilipokuwa nikitoka ndani ya basi la shule watoto walikuwa wananivuta na kunitupa katika [pipa la takatakana kunicheka , "alimwambia Jo Fidgen katika mahojiano na kipindi cha BBC " BBC Outlook. "
"Ilifika wakati ikambidi baba yangu awe ananisubiri kwenye kituo cha basin a kunisindikiza hadi nyumba, na watoto walinisumbua hata zaidi, huku wakinikejeli : 'Ha ha! Hebu tazama mwanaume huyo mzee mwenye takataka .'
Baba yake Figgers, Nathan, alikuwa na umri wa miaka 74 na mama yake, Betty May, 66 walipomuokota.
Walikuw ana watoto wao, na walikuwa wamewachukua watoto wengine kumi na wawili wa kulea kwa miaka kadhaa- wengi wao wakati wazazi wao walipokuwa gerezani - na walikuwa wamepanga kuacha kuwachukua watot zaidi wa kule kwasababu walikuwa wanazeeka .
Lakini ghafla Freddie akawasili.
Hakuwa na mtu yeyote aliyemtaka, kwahiyo wakamuasilina kumkuza kama mtoto wao.
Wakati Freddie alipoanza kuuliza maswali , Nathan aliyafananisha na historia yake.
"Alisema . 'Ninakwenda kukwambia ukweli bila kukuficha, mama yako mzazi alikutelekeza . Na mimi na Betty hatukutaka kukupeleka katika kituo cha kuwatunza watoto, tulikuasili. Nilijihisi kama takataka nakumbuka akinishika mabega na kuniambia , 'Usikubali hilo likuudhi .'
" Wazazi wangu walinipa upendo ambao yeyote angetaka apewe. Walinifanyia kila kitu. Sikuwahi kuhisi haja ya kuitafuta familia yangu ya damu kwasababu baba yangu na mama yangu , Betty wangu na Nathan wangu, walikuwa kila kitu kwangu . Niliwapenda. "
"Ni watu wazuri. Walinifunza kuwa na maadili, kufanya jambo sahihi, kutosahau nilipotoka. Nilimuona baba yangu kila mara akiwasaidia watu, akisimama njiani kuwasaidia watu wasiojulikana, akiwalisha watu wasio na makazi ...

No comments:
Post a Comment