Klabu ya soka ya Simba SC imemteuwa Fatema Gulamabbas Dewji kuwa mlezi wa timu ya soka ya wanawake ya Simba Queens.
Uteuzi huo umetangazwa na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo Barbara Gonzalez, kwenye mkutano mkuu wa wanachana uliofanyika leo Februari 7, 2021 katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es salaam.
Barbara ameeleza kuwa Fatema ni mtaalam wa Masoko pamoja na kukuza chapa, hivyo anatarajia ataifikisha mbali Simba Queens.
''Napenda kumtambulisha Fatema Gulamabbas Dewji kuwa ndio mlezi wa timu yetu ya wanawake Simba Queens. Ni mtaalam wa masoko na kukuza chapa na kikubwa ni shabiki mkubwa wa Simba SC'' - Barbara Gonzalez
Akiongea mbele ya wanachama kwenye Mkutano Mkuu huo mara baada ya kutangazwa, Fatema amesema atatumia uzoefu wake wa masuala ya masoko kuhakikisha anawasaidia wachezaji kutambulika Tanzania na duniani kiujumla.
Pia amesema moja ya vipaumbele vyake vikubwa ni kuhakikisha Simba Queens inatetegea ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara.

No comments:
Post a Comment