Search This Blog

Wednesday, February 3, 2021

DC Jokate azindua tamasha la Utalii Kisarawe

 


Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amezindua tamasha la Utalii ndani ya Wilaya ya Kisarawe liitwalo 'Kisarawe Ushorobo Festival', litakalofanyika ndani ya siku tatu mfululizo ambapo litaanza rasmi tarehe 19 mwezi huu likijumuisha wasanii wa muziki, wachonga vinyago, ngoma za asili, wapishi wa vyakula vya asili (wazaramo), wakimbiaji n.k

Tamasha hilo limelenga kukuza sekta ya Utalii Wilayani kisarawe kupitia vivutio mbalimbali vilivyopo katika wilaya hiyo kama Msitu wa hifadhi ya mazingira asilia pugu kazimzumbwe.

Akizunguma leo wa waandishi wa habari, #DCJokate amesema kuwa tamasha hilo la Kisarawe Ushorobo Festival pia limelenga kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli za kukuza sekta ya utalii hapa nchini.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...