Search This Blog

Friday, February 5, 2021

Biden akatiza msaada wa Marekani kwa muungano wa kijeshi nchini Yemen


Rais wa Marekani Joe Biden ametangaza jana kuwa serikali yake inasimamisha msaada kwa mashambulizi ya kijeshi yanayoongozwa na Saudia Arabia nchini Yemen ambayo yameongeza mateso katika taifa hilo na kuitaja hatua hiyo kama sehemu ya Marekani ya kudumisha msisitizo wa nchi hiyo kuhusu diplomasia, demokrasia na haki za binadamu.

Wakati wa ziara yake ya kwanza katika wizara ya mambo ya nje kama rais, Biden aliwaambia wanadiplomasia kuwa vita hivyo vimesababisha janga la kibinadamu na la kimkakati na kwamba lazima vimalizike.

 Maamuzi hayo kuhusu Yemen ni moja kati ya mikakati iliyotolewa na Biden hapo jana ambayo amesema inalenga kubadilisha mwelekeo wa sera ya mambo ya nje ya Marekani. 

Tangazo hilo pia linatimiza ahadi ya kampeni za Biden lakini pia linaonyesha Biden akiangazia mgogoro mkubwa wa kibinadamu ambao Marekani imechangia kuuchochea. Hatua hiyo pia inawakilisha ukosoaji kwa Saudi Arabia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...