Search This Blog

Saturday, January 2, 2021

Yanga Manyara yafunga mwaka Kibabe,wawaalika Simba


Na John Walter-Manyara.

Wanachama wa Tawi la Klabu ya soka ya Yanga SC mkoa wa Manyara wamemaliza mwaka 2020 kwa kula na kunywa huku ikiwaalika watani wao wa jadi Simba sc tawi la Manyara.

Wanachama hao wamesheherekea mwaka mpya 2021  timu yao ikiwa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu soka Tanzania, ikiwa na pointi 44, baada ya kutoka sare ya 1-1 na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa raundi ya 18 mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

Mwenyekiti wa tawi la Yanga mkoa wa Manyara Ibrahim Kenju amesema wameamua kufanya sherehe ya mwaka mpya kwa kundelea kushambulia kwa kasi na mashambulizi yao yakazaa matunda dakika ya 76 kwa kupata goli la kusawazisha kupitia kwa Saidi Ntibazonkiza.

Kwa upande wa Simba sc, Mwenyekiti wa tawi mkoa wa Manyara Haji Athumani amesema jambo walilofanya Yanga wameiga kwa sababu wao ndio waliotangulia kufanya hivyo wakati wakifungua tawi lao mwaka Jana.

'Sisi tulianza kufanya hivyo tulichinja ng'ombe,hawa wameig, sisi mipango yetu mwaka 2021 ni kutembelea makundi yenye uhitaji na tunaanza na na kituo cha kulea watoto yatima wilayani Hanang'.

Hafla hiyo iliruhudhuriwa na Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Babati Fortunatus Fwema ambaye alisisitiza ushirikiano kwa mashabiki hao wa timu hizo mbili zenye historia kubwa katika nchi.

Fwema amesema Yanga Sc ilianzishwa enzi hizo kwa lengo la kutafuta Uhuru wa nchi huku Simba sc ikianzishwa na wakoloni wa Uingereza kwa ajili ya kuipinga Yanga, ikiitwa Queen Rangers.

Tawi la Yanga lilizinduliwa rasmi Tarehe 17/12/2020 na Kocha mkuu wa Yanga Sc  kocha ni Cedric Kaze kutoka Burundi.

Viongozi wa tawi la Yanga Manyara Mwenyekiti ni Ibrahim Kenju, Makamu Mwenyekiti Oswald Kambelende, Keneth Makotha (Katibu), Anna Kamafa (Mhasibu) Wajumbe ni Sauda Jumanne , Happy Masawe, Swalehe Carlos, Ziara Yassin Mfinanga na Ismail Mkungii.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...