Search This Blog

Friday, January 8, 2021

Waziri wa afya wa Ujerumani atafakari kuwania ukansela


Waziri wa afya wa Ujerumani Jens Spahn anatafakari kuingia katika kinyang’anyiro cha kugombea wadhifa wa kansela wa Ujerumani kwa niaba ya mfungamano wa vyama vya kihafidhina vya Christian Democratic Union,CDU na Christian Social Union CSU.

Taarifa hiyo imetolewa na gazeti maarufu la Ujerumani “Bild”. Kansela Angela Merkel amesema hatagombea muhula wa tano kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini Ujerumani mnamo mwezi Septemba. 

Wakati huo huo chama hicho cha CDU cha Kansela Merkel kinatarajia kumchagua mwenyekiti mpya wiki ijayo. 

Mshindi wa atakuwa na uwezekano mkubwa wa kugombea ukansela. Hata hivyo mtu mwengine pia anaweza kugombea ukansela.

 Kwa mujibu wa taarifa ya gazeti la “Bild” waziri wa afya Jens Spahn ambaye amekuwa maarufu zaidi, kutokana na juhudi za kupambana na maabukizi ya virusi vya corona amekuwa anajadili mustakabal wake wa kisiasa na viongozi muhimu wa chama cha CDU.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...