SERIKALI imepiga marufuku wananchi wa kanda ya ziwa kula nyama ya nguruwe ikiwa ni hatua za kukabiliana na mlipuko wa homa ya nguruwe uliotokea hivi karibuni.
Aidha imewaagiza wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi kuhakikisha wanasimamia kikamilifu karantini zilizowekwa kwaajili ya kutibu nguruwe ambao tayari wameathirika na ugonjwa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini hapa Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki alisema taarifa zilizopo zinaonyesha homa ya nguruwe ilianzia kwenye halmashauri 6 ya kanda ya ziwa.
"Kutokana na uwepo wa homa ya nguruwe tumewataka wananchi wa kanda ya ziwa kuacha kula nyama ya nguruwe ilikukabiliana na ugonjwa huu hatari ambao hauna tiba wala kinga,
" Nawaagiza viongozi mnaohusika mikoani na wilayani kuhakikisha mnasiamia karantini zilizowekwa kwa lengo la kuhakikisha kuwa ugonjwa huu hausambai kwenda maeneo mengine na kuleta madhara"alisema
Waziri Ndaki alizitaja halmashauri ambazo hazitaruhusiwa kula nyama ya nguruwe kuwa ni Mbogwe,Sengerema,Geita,Misungwi,Kyerwa na kahama ambazo kwa kiasi kikubwa zimeathilika na ugonjwa huo.
Alisema hadi kufikia januari 22 mwaka huu zaidi ya nguruwe 1500 sawa na asilimia 10 ya nguruwe wote nchini wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.
"Serikali inaendelea kufuatilia na kufanya kila linalowezekana kuhakikisha ugonjwa huu unadhibitiwa haraka iwezekanavyo iliusienee katika maeneo mengine na kusababisha hasara kwa wafugaji wengi zaidi" alieleza
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Magonjwa ya Mifugo Tanzania Ezron Nonga alisema lengo la kuzuia wananchi kula nyama ya nguruwe ambayo imeathirika na ugonjwa huo ni kudhibiti usienee kwa kasi katika maeneo mengine ambayo bado hayajaathilika
Aliwataka wafugaji wahakikishe wanatoa taarifa za ugonjwa au vifo vya nguruwe Mara vinapotokea, na pindi wanapokufa kuhakikisha wanazikwa kwa kuchimba shimo refu au kutekezwa kwa moto
"Ugonjwa wa homa ya nguruwe huanzia kwa nguruwe pori na baadaye husambaa kwa nguruwe wa kufugwa kwa njia ya kugusana,damu,mate,kinyesi na maji maji mengine yanayotoka kwa wanyama wagonjwa au kugusa vifaa vyenye maambukizi" alieleza

No comments:
Post a Comment