Watu 159 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na virusi vya corona (covid-19) ndani ya masaa 24 nchini Uturuki.
Idadi ya watu waliofariki kwa virusi vya corona (covid-19) tangu kuzuka kwa janga hilo hadi kufikia sasa nchini Uturuki imefikia 24,487.
Jumla ya watu 168,894 waliweza kufanyiwa vipimo vya covid-19 ndani ya siku moja ambapo kesi 752 ziligundulika. Idadi ya kesi za maambukizi ndani ya siku moja imefikia 6435.
Idadi ya waliopona imefikia 2,283,919 ikiwa ni pamoja na watu 5932 walioruhusiwa kuondoka hospitali.
Kwa upande mwingine, Waziri wa Afya Fahrettin Koca amesema kuwa chanjo ya raia wenye zaidi ya umri wa miaka 85 itaanza leo.
Koca alisema katika taarifa baada ya mkutano na Kamati ya Sayansi
"Tunasisitiza masharti yote kuhakikisha kuwa raia wetu wengi wanafika kwenye chanjo haraka iwezekanavyo."

No comments:
Post a Comment