Search This Blog

Wednesday, January 20, 2021

Watu zaidi ya milioni wapewa chanjo Uturuki


Nchi ya Uturuki ambayo ilizindua mchakato wa chanjo dhidi ya corona (Covid-19) siku ya Alhamisi tarehe 14 Januari, imetoa chanjo kwa watu zaidi ya milioni moja hadi kufikia sasa.

Katika awamu ya kwanza ya mchakato wa chanjo iliyoanzishwa kote nchini, wataalamu wa huduma za afya walipokea dozi ya kwanza ya chanjo ya CoronaVac iliyozalishwa na kampuni ya Sinovac kutoka China.

Sambamba na hatua ya pili ya awamu ya kwanza, chanjo zilianza kutolewa kwa wahudumu wa nyumba za wauguzi, vituo vya walemavu na walezi pamoja na raia wenye umri wa miaka 90 na zaidi.

Katika siku ya saba ya chanjo, takwimu zimeonyesha kwamba zaidi ya watu milioni moja walipewa dozi ya kwanza ya chanjo ya CoronaVac.

Baada ya awamu ya kwanza kumalizika, awamu ya pili ya chanjo itaanza kutolewa siku 28 baadaye.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...