Search This Blog

Sunday, January 10, 2021

Watu watatu wauwawa katika shambulizi la bomu Afghanistan

 


Mlipiko wa bomu barabarani katika mji mkuu wa Afghanistan umesabisha vifo vya watu watatu na wengine kujeruhiwa. Shambulizi hili linajiri wakati ambapo wawakilishi wa mazungumzo ya amani kati ya Afghanistan na Taliban wako Qatar kujadili kuundwa kwa serikali ya mpito. 


Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Tariq Arian, amesema miongoni mwa waliuwawa katika shambulizi hilo ni msemaji wa kikosi cha ulinzi wa umma Zia Wadan pamoja na wafanya kazi wenzake wawili. Inaarifiwa kuwa bomu hilo lililenga kushambulia gari la msemaji huyo wakati wa pilka pilka za barabarani za asubuhi jumapili ya leo. 


Kufikia sasa hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na shambulizi hilo, lakini Rais Ashraf Ghani amelishutumu kundi la Taliban kuhusika. Vurugu zinaendelea kuongezeka Afghanistan hasa katika miezi ya hivi karibuni huku mashambulizi yakitekelezwa kulenga wanasiasa, wanahabari na wanaharakati wa kutetea haki za binaadam licha ya mazungumzo kuanza kati ya serikali ya Afganistan na Taliban.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...