Search This Blog

Saturday, January 9, 2021

Wanasiasa waonywa kukwamisha shughuli za maendeleo


Na Timothy Itembe Mara.

Wanasiasa waonywa kuacha Siasa katika swala zima linalogusa maendeleo ya wananchi kwa kutaka kukwamisha lisifanikiwe.

Mtendaji wa mtaa wa Mkutuni kata ya Turwa,Elya Mgusuhi alibainisha mbele ya mwaandishi wa habari hizi kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanatumia nafasi walizonazo kutaka kukwamisha shuguli mbalimbali za maendeleo ya wananchi ili zisifanikiwe.

Mtendaji huyo alisema kuwa katika harakati za kuona swala la shule ya Turwa sekondari mpya inayojengwa katika kata hiyo ambayo imefikia hatua nzuri kuna baadhi ya wanasiasa wanajitokeza kufanya siasa ili ujenzi huo usifanikiwe na watoto kukwama katika swala zima la kuanza masomo wakati shule zinafunguliwa.

"Mimi niseme  kuwa kuna baadhi ya wanasiasa ambao wanatumia ndimi zao vibaya katika kuhakikisha kuwa swala zima la maendeleo kwa Wananchi ambapo alionya kuwa kufanya hivyo hakukubaliki na kuwa nikosa kisheria kukwamisha shuguli za maendeleo kwa namna yeyote ile"alisema Mgusuhi.

Afisa hiyo aliongeza kuwa shule hiyo inajengwa baada ya wanafunzi waliofaulu kukoswa nafasi ya kujinga kidato cha kwanza mwaka 2020/2021.

Mgusuhi alimaliza kwa kusema kuwa shule hiyo ya Turwa Sekondari inatarajia kupokea wanafunzi zaidi ya 212 ili kusoma hapo na kupunguza umbali wa wanafunzi kutembea mwendo mrefu wakifata masomo shule za Rebu,Nkende na kwingineko.

Naye diwani kata ya Turwa Chacha Marwa Machugu alimaarufu(MUSUKUMA) alitumia nafasi hiyo kumwagia sifa wadau wa maendeleo waliochangia na kuhakikisha shule hiyo inakamilika na watoto wanaanza masomo ifikapo mda wa kufunguliwa.

Musukuma aliongeza kusema,pongezi nyingi zimwendee mkurugenzi wa halmashauri ya Tarime mjini,Elias Ntiruhungwa kutoa mchango wa mabati pia kamati ya mfuko wa jimbo kutoa mifuko ya Saruji 100,nondo milimita 12 pc30 na milimita 6 pc 10 na mahitaji mengine.

Katika upande wa wenyeviti wa mitaa minane mwenyekiti wa mtaa KebikiriJuma Gidion kwa niaba ya wenzake alisema kuwa shule hiyo inajengwa kwa ushirikiano mkubwa isipo kuwa kuna baadhi ya wanasiasa wanatumia nafasi hiyo kutaka kukwamisha shugulihiyo isifanikiwe.

Gidion aliongeza kusema kuwa wenyeviti katika kuhakikisha shule hiyo inakamilika wametumia nafasi walizo nazo kuhamasisha jamii kuchangia shuguli za maendeleo huku wakitoa fedha zao pamoja na nguvu kazi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...