Search This Blog

Thursday, January 14, 2021

Wafanyabiashara waomba WhatsApp na Facebook vizuiwe


Shirikisho la wafanyabiashara wa India (CAIT) limeiomba Serikali izuie mtandao wa WhatsApp, Facebook na Facebook Messenger kutokana na sera mpya ya Faragha.

Wamemuandikia Waziri wa Habari na Teknolojia kuwa India ina watumiaji zaidi ya milioni 200 hivyo kuchukua taarifa zao kwa matumizi ni hatari kwa uchumi wa nchi.

Aidha, wamesema kuchukua taarifa za manunuzi na taarifa nyingine sio mbaya tu kwa Uchumi bali pia hata usalama wa nchi unaweza kuwa mashakani.

CAIT wamesema sera mpya ya faragha ya WhatsApp inakiuka misingi ya faragha na ipo kinyume na masuala ya msingi yaliyo kwenye Katiba ya India.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...