Search This Blog

Tuesday, January 12, 2021

Wademocrat Marekani wafungua rasmi mashtaka kumuondoa Trump madarakani


Wabunge wa chama cha Democratic nchini Marekani wamefungua rasmi mashtaka bungeni dhidi ya Rais Donald Trump kwa lengo la kutaka kumuondoa madarakani wakimtuhumu kwa kuchochea uvamizi wa majengo ya bunge Capitol Hill wiki iliyopita mjini Washington.

Hapo jana, Wademocrat waliwasilisha azimio katika Baraza la Wawakilishi kumtaka makamu wa rais Mike Pence kutumia ibara ya 25 ya katiba ya nchi hiyo kumtimua Trump madarakani kwa msingi kuwa hafai kuwa ofisini.

Lakini wabunge wa chama cha Republic walizuia azimio hilo kupitishwa moja kwa moja, na ndipo Wademocrat wakawasilisha mashtaka ya uchochezi dhidi ya Trump.

Hatua hiyo inayolenga kuyazima matarajio ya siku za baadaye ya Rais Trump kujihusisha katika siasa, inaweza kuwa kilele cha kile kimekuwa miaka minne ya malumbano kuelekea kuapishwa kwa Joe Biden kuwa rais mpya Januari 20.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...