Utafiti wa awali unaonesha kuwa virusi vipya vya ugonjwa wa corona vilivyojitokeza Uingereza ndio hatari zaidi, amesema Waziri mkuu Boris Johnson.
Data hiyo imetokana na kulinganishwa kwa idadi ya vifo kati ya watu waliopata maambukizi na virusi vipya ama vile vya zamani vya corona.
Maambukizi yanayosababishwa na virusi vipya tayari yamesambaa kote Uingereza.
Bwana Johnson amesema katika taarifa: "Mbali na kwamba vinasambaa kwa haraka, sasa hivi pia inaonekana kana kwamba kuna ushahidi kuwa virusi vipya - vile ambavyo mara ya kwanza kabisa vimebaini London na kusini mashariki - huenda vikahusishwa na idadi ya juu ya vifo.
"Yaani athari kubwa imetokana na virusi hivyo vipya na hilo linamaanisha wizara ya afya sasa hivi inakumbana na shinikizo kubwa."
Kundi lililokuwa linafanya utafiti, limehitimisha kuwa "kuna uwezekano mkubwa" virusi hivyo vimekuwa hatari mno.
Alisema: "Nataka kusisitiza kuwa bado kuna sintofahamu kuhusiana na idadi na juhudi zaidi zinahitajika lakini bila shaka inatia wasiwasi kwamba virusi hivyo vimechangia ongezeko la idadi ya vifo pamoja na kiwango chake cha maambukizi."
Uchunguzi wa awali umeonesha kuwa virusi vipya vinasambaa kwa asilimia 30 na 70 haraka zaidi ya virusi vyingine na inasemekana kuwa ni hatari zaidi kwa asilimia 30. Virusi hivyo vipya mara ya kwanza vimebainika Kent mnamo mwezi Septemba. Na sasa hivi vinapatikana kwa nchi zaidi ya 50 maeneo ya England na Ireland Kaskazini.
Chanjo za kampuni ya Pfizer na ile ya AstraZeneca ya Oxford - zote zinatarajiwa kuwa na ufanisi dhidi ya virusi hivyo vipya ambavyo vimejitokeza nchini Uingereza.
Hata hivyo, Sir Patrick, mshauri mkuu wa serikali juu ya masuala ya sayansi, amesema kuna wasiwasi kuhusu virusi vingine viwili ambavyo vimejitokeza Afrika Kusini na Brazil.

No comments:
Post a Comment