Vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati vimedai kurejesha udhibiti wa mji ambao awali ulikamatwa na waasi katikati ya taifa hilo.
Mji huo ulichukuliwa na waasi ambao walijihami kwa silaha mapema mwezi huu. Waasi hao wanaipinga serikali ya rais Faustin Touadera.
Msemaji wa serikali ya Touadera Vladimir Monteiro amesema mji wa Bangassou uko chini ya udhibiti kamili wa MINUSCA na kuongeza kuwa waasi waliutelekeza mji huo baada ya kupewa muda na vikosi hivyo siku ya Ijumaa.

No comments:
Post a Comment