Search This Blog

Friday, January 1, 2021

Vikosi vya Israel vyajeruhi Wapalestina


Vikosi vya Israel vimeripotiwa kuwajeruhi Wapalestina 16 kwa risasi za plastiki na kuathiri wengi kwa mabomu ya machozi, wakati wa makabiliano na waandamanaji waliotaka kufanya maandamano ya kupinga makazi ya haramu ya Wayahudi katika Ukingo wa Magharibi.

Wapalestina hao waliokusanyika kwa ajili ya maandamano ya dhidi ya makazi ya walowezi wa Kiyahudi katika vijiji vya Deyir Jarir vilivyoko karibu na mji wa Ramallah, walikita mahema kwenye milima na kukaa mkoani humo.

Vikosi vya Israel vilikabiliana na Wapalestina hao kwa kutumia risasi za plastiki na mabomu ya machozi ili kuwatawanya.

Vyanzo vya habari vimearifu kwamba vikosi vya Israel viliwajeruhi Wapalestina 16 kwa risasi za plastiki, na kuathiri wengi kwa mabomu ya machozi.

Taarifa zaidi zimefahamisha kuwa vikosi vya Israel vilitumia vyombo vya drone kutoa mabomu ya machozi, na baadaye  majeruhi walitibiwa na timu za matibabu za Wapalestina katika eneo hilo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...