Search This Blog

Friday, January 15, 2021

Urusi kumkamata Navalny kama atarejea Jumapili


Idara ya magereza nchini Urusi imesema italazimika kumkamata mara moja kiongozi wa upinzani Alexei Navalny iwapo atarejea nchini humo Jumapili kama alivyopanga. 

Idara hiyo imedai kuwa mkosoaji huyo mkubwa wa Rais Vladmir Putin alikiuka masharti ya kifungo chake. Navalny kwa sasa yuko Ujerumani tangu alipopewa sumu inayoharibu mishipa ya fahamu mwezi Agosti mwaka 2020. 

Navalny, mwenye umri wa miaka 44 aliugua akiwa ndani ya ndege akitokea Siberia kwenda Moscow na baadae alipelekwa Berlin kwa matibabu.

 Kiongozi huyo wa upinzani anadai kuwekewa sumu na Putin, madai ambayo yamekanushwa na Ikulu ya Urusi. 

Idara hiyo ya magereza imesema tayari imeiomba mahakama ya Moscow ibadilishe hukumu yake kuwa kifungo gerezani. 

Aidha, inadai Navalny alikiuka masharti mara sita kwa kushindwa kujisajili kwa maafisa mwaka uliopita, kama sehemu ya hukumu ya kifungo cha nje iliyotolewa mwaka 2014.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...