Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa huenda likakutana wiki Ijayo, kujadili misukosuko iliyomfika kiongozi wa upinzani anayeshikiliwa na polisi nchini Urusi Alexei Navalny, hatua inayohatarisha kuzuka mvutano na serikali ya nchi hiyo.
Kulingana na wanadiplomasia mkutano huo umepangwa kufanyika siku ya Jumatano baada ya mkutano wa mwezi utakaozungumzia vita vya Syria.
Mkutano huo ulikuwa umepangiwa kujadili kisa cha Navalny kupewa sumu mwaka uliopita lakini baadhi ya wanadiplomasia wanasema huenda wakajadili hali ya Navalny kwa sasa ambapo anashikiliwa na serikali ya Urusi kuanzia tarehe 17 Januari, baada ya kurejea nchini humo kutoka Ujerumani alikopelekwa kwa matibabu baada ya kupewa sumu.
Waandamanaji nchini Urusi na katika mataifa mengine ikiwemo Marekani na mataifa ya Umoja wa Ulaya wanataka Navalny mkosoaji mkubwa wa serikali ya rais Vladimir Putin aachiliwe huru.

No comments:
Post a Comment