Utawala wa Falme za Kiarabu (UAE) umeahirisha makubaliano ya msamaha wa viza waliofanya na Israel hadi tarehe 1 Julai.
Katika taarifa iliyoandikwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, iliarifiwa kwamba UAE imechukuwa uamuzi huo kutokana na janga la virusi vya corona (Covid-19).
Katika taarifa hiyo, kulitolewa tahadhari ya kuhusu suala la viza kwa raia wa Israel waliopanga kusafiri UAE ifikapo tarehe 1 Julai.
Kutokana na ongezeko la kesi za maambukizi ya Covid-19 kwa raia wengi wa Israel waliotembelea UAE, utawala wa Tel Aviv uliwataka wale wanaorudi kutoka nchi hii wakae karantini kwa wiki mbili katika hoteli zilizoteuliwa.
Utawala wa UAE uliidhinisha makubaliano ya msamaha wa viza na Israel mnamo Januari 13.
Chini ya makubaliano hayo, kuanzia Februari 13, raia wa Israel wangeweza kusafiri kwenda UAE bila viza.
No comments:
Post a Comment