Search This Blog

Friday, January 29, 2021

Tetesi za soka kimataifa

 


Paris St-Germain itafikiria kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, mwisho wa msimu huu iwapo mshindi huyo wa kombe la dunia atakataa kuandikisha kandarasi mpya na klabu hiyo. Klabu ya Liverpool na ile ya Real Madrid zina hamu ya kumsaini mshambuliaji huyo hatari. (Marca - in Spanish)

West Ham Itabadilisha kandarasi ya mkopo ya kiungo mshambuliaji wa Algeria Said Benrahma kutoka Brentford na kumsajili kwa kandarasi ya kudumu. West ham ililipa dau la £4.25m kumnunua mchezaji huyo kwa mkopo na italipa dau la £21.75m kumnunua mchezaji huyo.. (Eurosport)

Chelsea ina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Borrusia Dortmund mwenye umri wa miaka 20 Erling Haaland Kutoka klabu ya Borussia Dortmund pamoja na beki wa Bayern Munich raia wa Austria David Alaba, 28, mwisho wa msimu huu .

Mchezaji huyo ambaye ni mzaliwa wa eneo la Leeds lakini mwenye uraia wa Norway, Haaland ambaye anaweza kuondoka katika klabu hiyo iwapo dau la £66m litalipwa , ananyatiwa na Real Madrid ambayo pia ni klabu ambayo inamsaka Alaba. (Sky Sports)

Beki wa Arsenal na England Ainsley Maitland-Niles, 23, yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo ili kupiga jeki nafasi yake ya kushirikishwa katika kikosi cha England cha mashindano ya Ulaya yatakayofanyika majira ya joto. (Mirror)

Mkufunzi mpya wa Chelsea Thomas Tuchel hana mpango wa kuwasajili wachezaji wapya katika kipindi kilichosalia cha dirisha la uhamisho. (Goal)

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amesema kwamba atafikiria uwezekano wa kuongeza muda wa kandarasi ya mkopo ya Martin Odegaard ili kusalia katika klabu hiyo zaidi ya msimu huu baada ya kujiunga na klabu hiyo kutoka Real Madrid. (Times, subscription required)

Liverpool inatarajiwa kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 16 kiungow a Derby Kaide Gordon, ambaye ameiwakilisha England katika kiwango ha wachezaji wasiozidi umri wa miaka . (Goal)

Newcastle United ina hamu ya kumsaini tena beki Jetro Willems baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuhudumu kwa mkopo katika klabu hiyo msimu uliopita kutoka klabu ya Eintracht Frankfurt. (Chronicle)

Ujerumani itamuita kiungo wa kati wa Bayern Munich Jamal Musiala, 17, katika kikosi kikuu cha Ujerumani ili kumzuia kuichezea timu ya taifa ya England. Musiala amehudumu miaka minane na Chelsea , England katika timu isiozidi wachezaji wa umri wa miaka 21 . (Times, subscription required)

Mkufunzi wa Leeds United na Argentina Marcelo Bielsa, 65, atasubiri hadi mwisho wa msimu kabla ya kufungua mazungumzo ya kandarasi mpya.. (Mirror)

Manchester City inatarajia kupata zaidi ya £3m kutoka kwa mauzo ya asilimia 30 kufuatia uhamisho beki wa kulia wa Uholanzi Jeremie Frimpong, ambaye aliondoka Celtic na kuhamia Bayer Leverkusen kwa dau la £11.5m mapema wiki hii. Frimpong hakukichezea kikosi cha kwanza cha City kabla ya kujiunga na Celtic 2019. (Talksport)

Kiungo wa kati wa Fulham na Ivory Coast Jean Michael Seri, 29, anatarajiwa kujiunga na klabu ya Ufaransa Bordeaux kwa mkopo hadi mwisho wa msimu. (Guardian)

Stoke City inataka zaidi ya £15m ili kumuuza beki wake wa kati Nathan Collins, huku Arsenal na Burnley zikiwa miongoni mwa klabu zinazowakilisha jamhuri ya Ireland katika timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21. (Team Talk)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...