Search This Blog

Monday, January 25, 2021

Tetesi za soka kimataifa


 Edin Dzeko anatarajiwa kuondoka klabu ya Roma baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 raia wa Bosnia kutofautiana na mkufunzi Paulo Fonseca . (Goal)

Kurudi kwa Dzeko katika ligi ya Premia kunaweza kuwa suluhu kwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester City huku akitarajiwa kuondoka katika mji huyo wa Itali, huku klabu za Everton na West ham zikimmezea mate. (Gazzetta Dello Sport via Mail)

Mkufunzi wa West Ham David Moyes anamtaka kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard baada ya mkufunzi wa Red Devil Ole Gunnar Solskjaer kukubali kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kuondoka kwa mkopo. (Evening Standard)

Manchester United inafanyakazi ya kuzikabili klabu nyengine za Ulaya kama vile Manchester City, Barcelona na Juventus, kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 18 raia wa Brazil Gabriel Veron kutoka Palmeiras. (Sport via Star)

Mkufunzi wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino anataraji kujiunga tena na kiungo wa kati Delle Alli. Maombi matatu ya Mabingwa hao wa Ufaransa kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 yamekataliwa , lakini Pochettino anaungwa mkono na klabu hiyo kuendelea kumnyatia. (The Athletic, subscription required)

Wakati huohuo, PSG wameripotiwa kumpeana kiungo wa kati wa Ujerumani Julian Draxler, 27, kwa mbadala wa mchezaji wa Arsenal na Ufaransa mwenye umri wa miaka 21 Matteo Guendouzi. (L'Equipe via Mirror)

Klabu ya ligi ya Serie A Udinese ipo katika mazungumzo na klabu ya Wolves kumsaini mchezaji wa Itali Patrick Cutrone, 23, kwa mkopo . Mshambuliaji huyo amekuwa hachezeshwi mechi katika uwanja wa Molineux tangu kuwasili kwa Willian Jose kutoka klabu ya Real Sociedad. (Express & Star)

Parma pia ina hamu ya kumsajili Cutrone, ambaye hadi hivi majuzi alikuwa akihudumu kwa mkopo katika klabu ya Fiorentina.. (Corriere dello Sport)

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Southampton Charlie Austin, 31, anasema kwamba Manchester United iliamua kumsajili beki wa Sweden Victor Lindelof, 26, badala ya beki wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk in 2017, wakati alipokuwa akiichezea klabu hiyo ya saints. (Talksport)

Liverpool inakaribia kuafikia makubaliano ya dau la £1m kumsajili kinda wa klabu ya Derby, 16 Kaide Gordon. Mchezaji wa timu ya England isiozidi wachezaji wa umri wa miaka 16 amehusishwa na uhamisho kuelekea Man United na Tottenham.(Liverpool Echo)

Shkodran Mustafi, 28,ameanza mazungumzo na Arsenal kuhusu kukamilisha kandarasi yake mapema. Mchezaji huyo wa Ujerumani amehusishwa na uhamisho wa kuelekea klabu ya Lazio na beki huyo pia amekuwa akivutia klabu za Ujerumani . (Football.London)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...