Arsenal imeafikia makubaliano ya kumsani kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard, 22, kwa mkopo kutoka kwa Real Madrid. (Mail)
The Gunners wamekubali kulipa dau la £1.8m kumsajili Odegaard lakini hawatakuwa na fursa ya kifungu cha kumnunua katika kandarasi hiyo (Times - subscription required)
Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atamruhusu mshambuliaji wa England Jesse Lingard, 28, kuondoka kwa mkopo wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari lakini uamuzi wa mwisho utafanywa na bodi ya klabu hiyo ya Old Trafford . (ESPN)
Real Madrid huenda wakawa na hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Norway na Borussia Dortmund ,20, Erling Braut Haaland, ambaye anatakiwa na Chelsea na Man United baada mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kusema kwamba anafurahia kualia Paris St-Germain. (Express)
Beki wa Manchester City' na Uhispania Eric Garcia, 20, na kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30 - wote wakiwa kandarasi zao zinakamilika mwisho wa msimu huu - wanalengwa na Barcelona licha ya mkufunzi wa klabu hiyo Ronald Koeman kukiri kwamba timu hiyo haipo katika nafasi ya kusajili wachezaji mwezi huu .. (Mirror)
Newcastle United inatarajiwa kuthibitisha uteuzi wa Graeme Jones kuwa kocha kumsaidia wa Steve Bruce, ambaye ameunga mkono usajili huo. (Telegraph - subscription required)
Hatma ya mshambuliaji wa Uturukji Cenk Tosun' katika klabu ya Everton ipo mashakani baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kuwachwa nje ya kikosi kitakachocheza dhidi ya Sheffield Wednesday katika kombe la FA siku ya jumapili . (Liverpool Echo)
Kiungo wa kati wa Uskochi Billy Gilmour, 19, huenda akandoka Chelsea kwa mkopo mwezi huu licha ya kuanzishwa katika kombe la FA katika mechi ya ushindi dhidi ya Luton Town, kulingana na mkufunzi Frank Lampard. (Mail)
Mkurugenzi wa Real Madrid Emilio Butragueno ameonekana kuthibitisha kwamba kiungo wa kati wa Croatia mwenye umri wa miaka 35 Luka Modric atasaini kandarasi mpya katika klabu hiyo . (Marca - in Spanish)
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp ameiomba bodi ya klabu hiyo kutokosa fursa ya kumsajili beki wa Austria na Bayern Munich David Alaba, 28, wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu huu . (Don Balon - in Spanish)
Liverpool inapigiwa upatu kumsaini mshambuliaji wa Derby County Kaide Gordon, 16, katika mkataba wenye thamani ya £1m, huku Man United na Tottenham zikiwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo wa england. (Telegraph - subscription required)
Kiungo wa kati wa na Uholanzi Donny van de Beek, 23, yuko tayari kusalia katika klabu ya Old Trafford licha ya kupatiwa fursa chache kushiriki katika klabu hiyo licha ya kujiunga na miamba hiyo ya England kwa dau la £40m mwisho wa msimu huu . (Times - subscription required)
Klabu ya Fenerbahce imewataka mashabiki wake kusaidia kukusanya fedha kufuatia kusainiwa kwa mchezaji wa zamani wa Ujerumani Mesut Ozil, 32, kutoka Arsenal. (Mirror)
No comments:
Post a Comment