Search This Blog

Friday, January 8, 2021

Simba yatuma salamu Mtibwa Sugar

 


MIRAJ Athuman, kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Simba amesema kuwa anaamini kwamba leo wataibuka na ushindi mbele ya Mtibwa Sugar. 

Simba itakutana na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi unaotarajiwa kuchezwa majira ya saa 8:15, Uwanja wa Amaan.

Msimu wa 2020, Simba ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo wa fainali na kuifanya timu hiyo kukosa Kombe la Mapinduzi. 

Sheva amesema:"Tunajua Mtibwa Sugar ni timu nzuri na inafanya vizuri ila tutapambana kupata ushindi,".



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...