Search This Blog

Monday, January 25, 2021

Rais wa Ethiopia kuwasili nchini leo


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi amesema kuwa leo Januari, 25 Tanzania inatarajia kupokea ugeni wa Rais wa Ethiopia Bi. Sahle-Work Zewde kwa ziara ya kikazi ya siku moja Wilayani Chato mkoani Geita.

Prof. Kabudi ameyasema hayo leo huko Chato wakati akizungumza na wanahabari kuhusu ujio huo wa rais wa Ethiopia ambapo amesema kuwa mahusiano ya Tanzania na Ethiopia yamekuwa ya shida na raha.

“Uhusiano wetu na Ethiopia umekuwa katika hali zote na ni mahusiano ambayo yalitengenezwa na waasisi wa mataifa haya mawili ambayo yamekuwa na manufaa kibiashara,” amesema Prof. Kabudi.

Mhe. Sahle-Work Zewde ni rais wa kwanza mwanamke nchini Ethiopia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...