Search This Blog

Tuesday, January 26, 2021

Putin: Maandamano ya kudai kuwachiwa Navalny ni kinyume cha sheria


Rais wa Urusi Vladmir Putin ameyaita maandamano yaliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita kudai kuwachiwa huru kwa mkosoaji wa serikali Alexei Navalny kuwa kinyume cha sheria na hatari. Putin, akijibu maswali kutoka kwa wanafunzi, amesema hakuna anayepaswa kutumia hatua zinazokwenda kinyume cha sheria ili kuendeleza maslahi yao wenyewe ya kisiasa.

 Polisi iliwakamata zaidi ya watu 3,500 wakati wa maandamano ya kitaifa Jumamosi. Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell ataizuru Urusi mapema mwezi ujao kuishinikiza serikali kuhusu kukamatwa kwa Navalny, wakati umoja huo ukitafakari uwezekano wa vikwazo vipya. 

Ziara hiyo imethibitishwa leo katika mkutano wa mawaziri wa Mambo ya Kigeni wa mataifa 27 wanachama waliojadili hatua za kuchukua dhidi ya Urusi kufuatia kukamatwa kwa Navalny na ukandamizaji uliofanywa dhidi ya waandamanaji.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...