Search This Blog

Thursday, January 28, 2021

Putin asema Urusi inataka mahusiano bora na Ulaya


Rais wa Urusi Vladimir Putin ametoa wito wa kuwepo mahusiano imara kati ya nchi yake na Umoja wa Ulaya akisema Ikulu ya Kremlin iko tayari kwa ushirikiano thabiti. 

Akuhutubia kongamano la uchumi duniani linaloendelea mjini Davos, Uswisi, Putin amesema Urusi na Ulaya zina historia inayofanana na zinapaswa kurejea enzi ya kuwa na ajenda ya pamoja. 

Ingawa hakufafanua ni kwa jinsi gani Urusi na Ulaya zinaweza kuimarisha ushirikiano, Putin amesema pande hizo mbili zinaweza kupata mafanikio iwapo zitamaliza tofauti zilizopo na kufanya kazi pamoja bila kulaumiana.

Wito wa kiongozi huyo unakuja wakati mamia kwa maelfu ya warusi waliandamana Jumamosi iliyopita kumunga mkono kiongozi wa upinzani Alexei Navalny ambaye kuwekwa kwake kizuizini kumezusha lawama na ukosoaji mkubwa kutoka mataifa ya magharibi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...