Search This Blog

Sunday, January 24, 2021

Polisi wa Urusi wachunguzwa baada ya waandamanaji zaidi ya 3000 kukamatwa

 


Zaidi ya waandamanaji 3,000 wamekamatwa na polisi nchini Urusi kufuatia maandamano ya kumuunga mkono kiongozi wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa serikali ya Urusi ambaye amewekwa kizuizini na polisi Alexei Navalny huku waendesha mashitaka wakichunguza uwezekano wa polisi kuhusika katika ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya waandamanaji hao. 

Polisi walipambana na waandamanaji hao mjini Moscow huku maelfu wengine wakimiminika barabarani kufuatia wito uliotolewa na Navalny wa maandamano dhidi ya utawala wa Rais Vladimir Putin. 

Alexei Navalny alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Moscow alipokuwa anarajea nchini kutoka Ujerumani alikokuwa anapata matibabu baada ya kisa cha jaribio la kuuawa kwa kupewa sumu Agosti mwaka uliopita. 

Kundi la uangalizi la maandamano ya upinzani limesema polisi imewakamata waandamani 3,324 katika miji kadhaa nchini Urusi huku watu 1,320 wakikamatwa mjini moscow na wengine 490 wakimatawa katika mji wa pili kwa ukubwa wa Saint Petersburg.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...