Msemaji wa Wanahabari wa Vatican Matteo Bruni, amesema ,
"Kama sehemu ya mpango wa chanjo ulioanzishwa na Jimbo la Jiji la Vatican, ninaweza kuthibitisha kwamba Papa Francis amepewa dozi ya kwanza cha chanjo."
Bruni amesema kuwa mtangulizi wa Papa Franciscus, mwenye umri wa miaka 93, Papa Benedict XVI, pia amepewa chanjo ya Covid-19.
Kampeni ya chanjo ya Covid-19 ilizinduliwa jana huko Vatican.
Papa Franciscus, katika mahojiano yaliyochapishwa mnamo Januari 9, alisema,
"Ninaamini kimaadili kwamba kila mtu anapaswa kupewa chanjo.
Hili ni chaguo la kimaadili kwa sababu sio tu afya yako na maisha yako hatarini, lakini pia na maisha ya wengine."

No comments:
Post a Comment