Search This Blog

Wednesday, January 13, 2021

Mwanamke pekee aliyekabiliwa na adhabu ya kifo amenyongwa Marekani


Lisa Montgomery - mfungwa pekee wa kike aliyekuwa anakabiliwa na hukumu ya kifo nchini Marekani- amenyongwa baada ya kutekeleza mauaji.

Alidungwa sindano ya sumu katika gereza la Terre Haute, Indiana, baada ya Mahakama ya Juu Zaidi nchini Marekani kuamua kuondoa agizo la kuzuia kunyongwa katika dakika za mwisho.

Kesi yake ilizua hisia kali baada ya mawakili wake kusema kwamba alikuwa na tatizo la kiakili lilitokana na kunyanyaswa akiwa mtoto mdogo.

Utafutaji majibu katika maisha ya muuaji

Mwanamke huyo aliyekuwa na umri wa miaka 52- alimnyonga mama mja mzito kabla ya kumkata tumbo na kumteka mtoto wake katika eneo la Missouri mwaka 2004.

Mhasiriwa Bobbie Jo Stinnett, aliyekuwa na umri wa miaka 23 - alitokwa na damu hadi akafariki.

Montgomery ni mfungwa wa kwanza wa kike nchini Marekani kunyongwa katika kipindi cha miaka 67 iliyopita.

Kwa mujibu wa walioshuhudia, mwanamke aliyekuwa amesimama karibu na Montgomery wakati wa kuaawa kwake, alimuondolea usoni barakoa aliyokuwa amevaa na kumuuliza ikiwa ana jambo la mwisho angelitaka kusema. Montgomery alijibu "la", na hakuna kitu kingine.

Hatua ya kunyongwa kwake iliahirishwa mara mbili - kwanza kutokana na janga la Covid-19 wakati huo na jaji - hadi Mahakama ya Juu zaidi ilipotoa uamuzi wa kutekelezwa kwa hukumu hiyo mapema Jumatano.

Siku ya Jumatatu jaji mjini Indiana alisitisha ghafla kutekelezwa kwa hukumu hiyo hadi pale kesi ya kuchunguza hali yake ya kiakili ilipofanywa.

Mawakili wake wanasema alizaliwa na ugonjwa ulioathiri ubongo wake na kuongeza kuwa alikuwa mgonjwa sana..

Akiwa mtoto alidhulumiwa kingono na kimwili na baba yake huku mama akimsafirisha kimagendo, jamaa za familia yake walisema.

Alipitia kipindi kirefu cha ghasia na mateso wakati wa utoto wake , mawakili wake wanasema.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...