Search This Blog

Saturday, January 16, 2021

Mwakamo Cup kuunda timu itayocheza ligi ngazi ya Wilaya

Na Omary Mngindo, Mlandizi.

MICHUANO ya kuwania kombe la Mbunge Jimbo la Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani (Mwakamo Cup), yatatumika kupata timu itayoshiriki Ligi ngazi ya Wilaya.

Michuano hiyo inayotaraji kutimua vumbi kuanzia Jan 20 mwaka huu kwa ngazi za Kata, uteuzi wa awali utaanzia ngazi za Vijiji na Vitongoji wataoteua wachezaji wataounda kombaini za Kata, zitazokuja kucheza ngazi ya Jimbo.

Michuano hiyo inayotaraji kushirikisha vilabu zaidi nya 80 kuanzia ngazi za Vijiji na Vitongoji katani humo, kutakuwa na Kamati maalumu itayoteua wachezaji bora wataoingia kombaini hizo, zitazokuja kucheza hatua ya Jimbo.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati inayosimamia ligi hiyo Nassoro Shomvi (Mbilinyi), akizungumza na Waandishi wa Habari mjini hapa ambapo alisema kuwa hatua hiyo inalenga kuwepo timu itayoshiriki ligi ya wilaya chini ya KIBAFA.

Alisema kwamba Kamati hiyo chini ya wataalamu Charles Kilinda aliyewahi kuitumikia Yanga na Ivan Chenga Katibu Mkuu Mstaafu wa klabu ya JKT Ruvu, wamedhamilia kufanikisha malengo hayo yaliyoasisiwa na Mbunge Michael Mwakamo.

"Ligi yetu ya Jimbo tumeipanga ianze rasmi Jan 20 ngazi za Vijiji kwenye Kata zinazounda jimbo, lakini hatuwezi kuzipangia Kata kama watakuwa na mipango mingine ya kusogeza japo siku mbili tatu si kwa zaidi ya siku tano," alisema Shomvi.

Alisema kuwa wamejipanga kuunda timu imara itayoshiriki Ligi ngazi ya Wilaya ya Kibaha, huku akisema kuwa miaka mingi Jimbo hilo halina timu inayocheza ligi ya wilaya hata Mkoa, ukiachilia Ruvu Shooting inayokipiga Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Aidha Mbilinyi amewaomba wadau wa michezo katika vijiji na vitongoji kujitokeza kuzisaidia timu zinazotokea kwenye maeneo yao, kwa lengo la kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu kwenye ushiriki huo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...