Search This Blog

Wednesday, January 13, 2021

Marekani na UN zahimiza Uganda kuheshimu haki za binadamu


Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema serikali yake imefungia mitandao ya kijamii nchini humo kuelekea uchaguzi wa rais ambao umepangwa kufanyika kesho Alhamisi.

Museveni aliyezungumza usiku wa kuamkia leo ameishutumu kampuni ya Facebook kwa kile alichokitaja kuwa ujeuri, baada ya kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii kufunga akaunti kadhaa zinazohusishwa na kampeni yake kutaka achaguliwe tena.

Museveni amesema ana uhakika serikali imefunga mitandao ya kijamii na amewaomba msamaha Waganda kwa hali hiyo.

Mwanadiplomasia mkuu wa Marekani barani Afrika Tibor Nagy pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, wameelezea wasiwasi wao kuhusu hatua hiyo na kuitaka Uganda kuheshimu haki za binadamu kuelekea uchaguzi huo. 

Akizungumza kuhusu mtandao wa Facebook, Museveni amesema ikiwa mtandao wowote unataka kufanya kazi Uganda, basi ni lazima utoe nafasi sawa kwa wote, lakini ikiwa unataka kuwa na upendeleo dhidi ya chama tawala basi hauruhusiwi.

Hakukuwa na jibu au kauli ya moja kwa moja kutoka kwa kampuni ya Facebook kuhusu hatua hiyo ya Rais Museveni.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...