Search This Blog

Tuesday, January 5, 2021

Mabosi wa Gwambina wameingia sokoni kusaka Kocha mpya

 


BAADA ya kuipandisha timu ndani ya Ligi Kuu Bara na kuiongoza Gwambina kwenye jumla ya mechi 17 ikiwa nafasi ya 14 na pointi zao 19 benchi la ufundi limefutwa kazi mazima.

Kwa sasa mabosi wa Gwambina wameingia sokoni kusaka mbadala wa makocha hao ambao ataendeleza gurudumu ndani ya kikosi hicho kinachotumia Uwanja wa Gwambina Complex.

Kocha Mkuu, Fulgence Novatus na msaidizi wake Athuman Bilal sasa wapo huru kujiunga na timu yoyote baada ya ajira zao kusitishwa rasmi Januari 4.

Mchezo wa mwisho kukaa benchi ilikuwa ni dhidi ya Biashara United ambapo ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Kwa sasa timu ipo mikononi mwa kocha Khassain Salum na Seleman Kisedi pamoja na viongozi wengine.

Mkurugenzi wa benchi la ufundi ndani ya Gwambina FC ni Mwinyi Zahera ambaye aliwahi kuinoa Yañga.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...