Search This Blog

Sunday, January 10, 2021

Maandamano ya dhidi ya Netanyahu yaendelea Israel


Licha ya tahadhari na hatua kali za karantini zilizowekwa nchini Israel kwa ajili ya corona (Covid-19), maelfu ya watu walifanya maandamano ya kumtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu ajiuzulu.

Waisrael wamekuwa wakiendeleza maandamano yao dhidi ya Netanyahu kutokana na kushindwa kusimamia kesi ya ufisadi na kudhibiti janga la Covid-19 nchini humo.

Maelfu ya waandamanaji kutoka Tel Aviv, walikusanyika na kuandamana mbele ya makao makuu ya Waziri Mkuu licha ya hatua kali za karantini zilizowekwa dhidi ya Covid-19, kuzunguka mitaa ya Magharibi mwa Jerusalem wakiwa wamebeba bendera na mabango.

Waandamanaji hao waliovaa fulana zenye maandishi yaliyosoma, "Waziri Mkuu wa Uhalifu", wakimaanisha Netanyahu, mara kwa mara waliimba "Bibi (Netanyahu) nenda nyumbani". "(Rais wa Marekani Donald) Trump ameenda, na sasa ni zamu yako  (Netanyahu) " na kumtaka Netanyahu ajiuzulu.

Nchi ya Israel ambayo imeathiriwa na wimbi la tatu la janga la Covid-19 na kukumbwa na mzozo wa ukosefu wa ajira unaoongezeka, kumekuwa kukifanywa maandamano dhidi ya Netanyahu na kuendelea kwa kipindi cha wiki 29.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...