Search This Blog

Saturday, January 9, 2021

Kim Jong-un aahidi kuendeleza mpango wa silaha za nyuklia Korea Kaskazini




Kiongozi wa Korea KaskazinKim Jong-un amesema sera za Marekani juu ya nchi yake "hazitawahi kubadilika"

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema kuwa Marekani ndio "adui wake mkubwa" na kwamba hatarajii nchi hiyo kubadilisha sera yake kwa Pyongyang - haijalishi nani ndiye atakayekuwa rais.

Akizungumza katika kikao nadra sana cha chama chake tawala cha Workers' Party, Bwana Kim pia ameahidi kupanua mpango wake wa silaha za nyuklia Korea Kaskazini na uwezo wa kijeshi wa nchi hiyo.

Alisema kuwa mipango ya utengenezaji nyambizi za nyukilia iko karibu kukamilika.

Matamshi yake yanawadia wakati ambapo Rais Mteule Joe Biden anajitayarisha kuingia madarakani.

Wachambuzi wanasema maneno ya Bwana Kim ni juhudi za kuongeza shinikizo kwa rais mteule wa Marekani ambaye ataapishwa Januari 20.

Bwana Kim alifurahia uhusiano mzuri kati yake na rais Donald Trump anayeondoka madarakani, hata ingawa ni hatua ndogo tu iliyopigwa katika majadiliano juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...