Kasisi wa kikatoliki nchini Ufilipino anatarajiwa kuifikishwa mahakamani akishitakiwakwa makosa ya " kuhamasisha umma kuuasi utawala " kuhusiana na madai ya njama ya kumpindua madarakani rais Rodrigo Duterte.
Padre huyo, Father Flavie Villanueva ni mkosoaji mkubwa wa "vita dhidi ya madawa ya kulevya", vya rais Duterte ambayo alivianzishwa Julai Julai 2016.
Tangu mapambano dhidi ya biashara ya mihadarati yaanzishwe nchini Ufilipino, maelfu ya watu wameuliwa na polisi.
Padre Flavie Villanueva ameshutumiwa pamoja na watu wengine 10 kwa kuwa miongoni mwa watu walioandaa misururu ya video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ambazo serikali ilisema ziliichafua sifa ya rais Duterte.

No comments:
Post a Comment