Na Timothy Itembe Mara.
KANISA la Roho kazi ya Messiha limefunga mwaka 2020 na kukaribisha mwaka mpya 2021 kwa kufanya maombezi ya kuponya Wagonjwa na kuombea Taifa la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Kadinari,Joseph Ariyo wa kanisa la Nyamwaga ililoko wilayani Tarime alisema kuwa walilazimika kufanya hivyo kutokana na kurudishia shukurani Mwezi Mungu kuwalinda na kumaliza mwaka 2020 na kumuomba katika utukufu wake kuwasogeza katika mwaka mwingine wa 2021.
Kanisa la roho kazi ya messiha afrika mashariki(ukanda wa maziwa makuu) lenye makao makuu mkoani mara,kijiji cha Ikoma wilayani Rorya limetumia siku mbili kufanya huduma hiyo huku likiwataka waumini kuendelea kumtegemea mwenyezi Mungu katika mambo yote kwani yeye anaweza badala ya kwenda kuwategemea wanadamu.
“Huduma ya maombezi hayo ya kitaifa yalishirikiasha waumini wa kanisa hilo na wasio waumini kuombea wagonjwa na wenye shida mbalimbali, na wenye kusumbuliwa na mapepo na magonjwa mbali mbali yaliyoshindikana kutibika hospitalini,hivyo watanzania wote walio fanikiwa kufika kwenye maombi hayo waliweza kubarikiwa na kuuona utukufu wa bwana”alisema Ariyo
Kadinari huyo alitumia nafasi hiyo kusimamia uchaguzi ndani ya kanisa hilo ambapo nafasi ya katubu mkuu wa kanisa iklichukuliwa na Samweli Amosi Atendo maarufu kama Samtetezi hayo yalifanyika baada ya aliyekuwepo Washton Maebo kufariki mwanzoni mwa mwezi Desemba mwaka 2020
Katika halfa hiyo kanisa hilo lilichukua nafasi ya kumuombea Rais awamu ya Tano John Pombe Magufuli kuendelea kumcha Mungu na Taifa lake ambapo alimtanguliza katika Ugonjwa wa Corona na ameshinda huku mataifa mengine yakijiuliza tumeshindaje vita hiyo.
Kanisa hilo limetumia nafasi hiyo kumuomba Rais Magufuli kuendelea kutanguliza Mungu mbele katika shuguli zake huku akiwajali watumishi wa Mungu ndani ya Taifa hili ambapo kufanya hivyo uongozi utakuwa rahisi kwani uongozi ni tunu kutoka kwa Mungu hata rais Mgufuli amechagul;iwa na Mungu alisema.
Baraka Biseko mkazi wa Kogaja wilayani hapo alishukuru kwa maombi ya siku mbili yaliyofanyika na kuomba kanisa hilo kuendelea kueneza Ijii ya Bwana ambapo piaalisema amebarikiwa na mkutano huo na kupata uponyaji wa Roho pamoja mwili na kuomba waumini waendelee kumtumainia Mwenyezi Muingu kwani ndiye anaweza kilajambo.

No comments:
Post a Comment