Search This Blog

Monday, January 18, 2021

Idadi ya waliofariki dunia Darfur yafikia 80


Madaktari nchini Sudan wanasema zaidi ya watu 80 wameuawa katika kipindi cha siku mbili katika mapigano kati ya makabila mawili hasimu eneo la Darfur.

Mamia ya wengine wamejeruhiwa wakati wa mapigano hayo huko El Geneina.

Kambi iliyo karibu ya watu waliolazimika kutoroka kwao pia ilishambuliwa wakati wa mapigano hayo ambayo ndio mabaya kutokea tangu kufikiwa kwa makubaliano ya amani Oktoba mwaka jana.

Walinda amani wa kimataifa walianza kujiondoa Darfur kwa awamu kuanzia mapema mwezi huu.

Ripoti zinasema kuwa vurugu zilianza pale mwanaume mmoja wa Kiarabu alipochomwa kisu hadi kufa na mwanaume mwingine ambaye si mwarabu na kusababisha ufyatulianaji wa risasi.

Serikali ya Sudan inatuma vikosi vyake vyake katika eneo hilo kulinga raia.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...