Vyombo vya habari nchini Tunisia vimeripoti kuwa ofisi ya Rais Kais Saied ilipokea kifurushi chenye sumu, hatua iliyosababisha mamlaka kufanya uchunguzi.
Kaka wa Rais, Naoufel Saied, amesema kwenye mtandao wa Facebook kuwa ''rais yuko salama'' bila kufafanua zaidi, kwa mujibu wa ripoti.
Tunisia iko katikati ya mtikisiko mkubwa wa uchumi na sekta yake ya afya pia inakabiliwa na changamoto kutokana na kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya Covid-19.
Kumekuwa na maandamano nchini humo kutokana na changamoto za kiuchumi.
Maandamano yalianza wakati wa kumbukumbu ya miaka 10 ya mapinduzi ya Tunisia, yaliyochocheza wimbi la mapinduzi katika nchi za Kiarabu.
No comments:
Post a Comment