Search This Blog

Tuesday, January 12, 2021

FBI yaonya wafuasi wa Trump huenda wakazua ghasia zaidi


Shirika la upelelezi la Marekani FBI, limeonya kuhusu uwezekano wa maandaamnao yenye silaha kufanywa kote nchini siku chache kabla ya Joe Biden kuapishwa kuwa rais.

Kuna ripoti ya makundi yaliojihami yanapanga kukusanyika katika mabunge ya majimbo yote 50 na Washington DC kuelekea siku ya kuapishwa kwake Januari 20.

Hofu hiyo inajiri wakati mipango ya usalama imeimarishwa kwa ajili ya hafla hiyo.

Siku ya Jumatatu Bw. Biden aliwaambia wanahabari kwamba haogopi kula kiapo chao urais nje ya bunge la Marekani.

Yeye pamoja makamu wake mteule Kamala Harris bado wanatarajiwa kuapishwa nje ya jumba la Capital Hill, wiki mbili baada ya eneo hilo kuvamiwa na wafuasi sugu wa Rais Trump wanaopinga matokeo ya uchaguzi.

Maafisa wa usalama wamesisitiza hali iliyoshuhudiwa Januari 6 haitarudiwa tena- baada ya maelfu ya wafuasi wa Trump kufanikiwa kuingia katika majengo hayo wakati wabunge walikuwa wakipiga kura kuidhinisha matokeo ya uchaguzi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...