Search This Blog

Friday, January 15, 2021

Dodoma Jiji yakamilisha usajili wa Manyika Junior

Klabu ya Dodoma Jiji inayonolewa na Kocha Mkuu,  Mbwana Makata imekamilisha usajili wa kipa wa zamani wa Klabu ya Polisi Tanzania Manyika Junior ambaye aliwahi kudaka ndani ya Klabu ya Simba. 

Manyika alikuwa ndani ya Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu,Malale Hamsini kwa msimu wa 2019/20-2020/21 alijiunga na Klabu ya Polisi Tanzania akitokea Klabu ya KCB ya Kenya.

Akiwa ndani ya Polisi Tanzania mkataba wake ulipomeguka msimu wa 2020 hakuongezwa mkataba mwingine hivyo amejiunga ndani ya Didoma Jiji akiwa ni mchezaji huru.

Anakuwa ni nyota wa pili kutambulishwa ndani ya Dodoma Jiji leo Januari 15 ambapo dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufungwa.

Mwingine ambaye ametambulishwa leo ni winga Erick Nkosi ambaye alikuwa akikipiga ndani ya Mwadui FC na wote wakiwa wamepewa dili la mwaka mmoja.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...